ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya Simba Mganda Moses Basena, amewasilisha tena barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akiitaka Sim,ba iketi naye na kumalizana naye,kinyume na hapo ataichukulia hatua za kisheria.
Simba ilimtupia virago kocha huyo aliyekuja kurithi mikoba ya Mzambia Patrick Phiri kutokana na kutokuwa na vyeti vya taaluma yake.
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema Basena abaye awali aliwasilisha tena barua ya malalamiko kwa
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji, alisema wamepokea barua hiyo ya pili toka kwa Basena akitoa angalizo hilo
Wambura amesema kuwa Basena ameomba TFF imsaidie katika kupata suluhu hiyo toka Simba kwa kuwa hana maelewano mazuri na viongozi wa klabu hiyo.