Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungua watu waliofika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu kushuhudia kombe la UEFA jijini Dar es salaam jana. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
WAKATI kombe la klabu bingwa Ulaya likitua nchini jana, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kuwa ujio wa makombe makubwa nchini ni kichocheo cha kuleta maendeleo katika mchezo huo.
Alisema kutokana na Tanzania kuwa moja ya nchi zinazopata bahati hiyo itasadia kuleta makubwa katika sekta ya mchezo huo.