MSANII wa muziki wa kizazi kipya toka kundi la Tip Top Connection, Ahmed Ally ‘Madee’ ameanza kurekodi video ya
wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Stori’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Madee alisema kuwa kazi ya
kurekodi video hiyo inafanywa na Adam Juma ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya
Visual Lab.
Alisema pamoja na kuanza kuufanyia video wimbo huo
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam bado hajauachia katika vituo
vya redio na atafanya hivyo hivi
karibuni.