CLIFFORD NDIMBO, MSEMAJI WA SIMBA
Ofisa Habari wa Simba, Clifford Ndimbo alisema mchezo mwingine utazishirikisha Simba Veterani na timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA) huku timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Simba itaumana na timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Azam.
Ndimbo alisema Simba itamenyana na Express ya Uganda baada ya michezo hiyo na burudani mbalimbali kuanza kabla ya mchezo huo.
Aidha siku hiyo itakuwa maalum kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wa Simba, uzinduzi wa jezi za nyumbani na ugenini, tovuti na kalenda ya timu hiyo kwa msimu mzima wa mashindano mbalimbali na kuitambulisha kampuni ya Push Mobile sambamba na promosheni ya kukwangua na ushinde ikiwemo kulipia malipo ya kupata taarifa za Simba kupitia huduma ya ujumbe mfupi wa maneno.
Alitoa wito kwa wachezaji maveterani wa Simba leo kujitokeza kwa ajili ya taratibu za mchezo wa siku ya Simba Day.
Ndimbo alitaja viingilio vya siku hiyo VIP ni shilingi 20,000, Jukwaa Kuu 12,000, main stand shilingi 8000 na mzunguko shilingi 4000.
“Tumewasilisha taarifa za siku hiyo kwa TFF ili siku hiyo itambulike katika kalenda ya Shirikisho hilo kuanzia mwakani,” alisema Kaijage.
hili ndilo timu la ukweli ambalo halifanani na jangwani, big up kwa Simba Day
ReplyDeletehalafu msemaji wetu ni wa ukweli, rage alitaka kumpoteza kwa kumpa asiyestahili, Ibarahim Masoud ambaye si mwake kuwa msemaji wa klabu kubwa kama Simba, Rage wakati mwingine asikurupuke
ReplyDelete