KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kiungo Mikel
Arteta atakosa mechi ya leo ya Ligi ya Mabingwa dhidi yan AC Milan.
Mchezaji huyo wa zamani wa Everton aliuamia kichwani kwenye
mechi dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, ambayo timu yake ilishinda
2-1 mwishoni mwa wiki baada ya kugongana na Jordan Henderson.
“Tumewapoteza Benayoun, Diaby na Arteta naye. Arteta anatakiwa
kupumzika kwa wiki moja. Rosicky yuko katika hatihati pia. Lakini tutashusha
kikosi kizuri ili kufuzu,”alisema Wenger.
Kocha wa The Gunners anajiamini kikosi chake kinaweza kufuzu
licha ya kutakiwa kufunga mabao manne.
“Tunaweza kufunga mabao. Katika mechi mbili zilizopita za
nyumbani tumefunga mabao 12. Lazima tujenge uwiano sawa katika kushambulia na
kuzuia.
“Kama Milan inaweza kufunga nne, tunaweza kufanya hivyo pia …
tunajua tunaweza kuonyesha kiwango kizuri.”
Mfaransa bado anaamini timu yake inaweza kuwakatamata Tottenham
katika Ligi Kuu licha ya wapinzani wao kuwa mbele kwa pointi nne, zikiwa
zimebaki mechi 11.
Pia anahisi timu yake haina cha kupoteza ikicheza na Milan leo,
lakini amekiri wanatakiwa kujitoa kwa kila kitu dhidi ya wapinzani wao hao
kwenye Uwanja wa Emirates.
“Nilisema, si jambo lisilowezekana [kuwakamata Tottenham] kwa
sababu tulitakiwa kucheza nao… tumekuwa mwendelezo,”alisema Wnger.