Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo
(kulia) akitoa tamko jana jijini Dar es salaam la kutaka Shirikisho la Soka
Nchini (TFF) kulipa Shilingi milioni 5 kwa ajili ya gharama za matengenezo ya
viti vya Uwanja wa Taifa vilivyoharibiwa na Washabiki wakati Mechi ya Simba na
Kiyovu wiki iliyopita. Uharibifu huo umesababisha viti 152 kuharibiwa na 11
kuvunjwa kabisa. Mkurugenzi huyo alitoa tamko hilo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana ,
Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi .Kushoto ni Afisa Habari Idara ya
Habari(MAELEZO) Lydia Churi.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam