Na Dina
Ismail
TANZANIA
imebahatika kuwa na wachezaji wenye vipaji mbalimbali kiasi cha kuweza kuiletea
sifa nje ya nchi kwa kutwaa ubingwa ama kushika nafasi za juu katika mashindano
mbalimbali.
Michezo kama
riadha, masumbwi, mpira wa kikapu, mbio za nyika, mpira wa wavu, kuogelea ni
baadhi tu ambayo tunaweza kujivunia wachezaji wake.
Licha ya
kutuletea sifa lakini michezo hiyo bado imekuwa haipewi kipaumbele kwa namna
moja ama nyingine kama ilivyo kwa mpira wa miguu.
Sote
tunaamini na kujiridhisha kwamba, mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana kiasi
cha kujizolea mashabiki wengi katika nchini nyingi duniani.
Kimafanikio,
hapa Tanzania hatuwezi jivunia mpira wa
miguu ukilinganisha na riadha au ndondi
ambayo mara kwa mara imekuwa ikituletea medali.
Lakini cha
ajabu soka ni mchezo ambao unathaminiwa zaidi na kupewa sapoti ya kutosha
katika kila sekta kila kukicha.
Kuna
makampuni, taasisi na hata watu binafsi hujitokeza kusapoti ama kudhamini mchezo
mpira wa miguu iwe katika ligi, mashindano ya ndani au nje, lakini si kwa
michezo nyingine.
Timu za michezo
kama ngumi au riadha hujikuta katika maandalizi duni kutokana na ukata lakini
hufanya maandalizi kufa kupona na hatimaye hushiriki na kushinda.
Mfano mwezi
uliopita, timu ya Taifa ya Tenisi kwa watu wenye ulemavu iliitoa kimasomamso
Tanzania baada ya kufuzu kucheza
mashindano ya kombe la dunia kwa mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika mwezi
Mei mwaka huu nchini Italia.
Timu hiyo
ilifuzu hatua hiyo bada ya kushika nafasi ya kwanza katika michuano ya Afrika iliyofanyika Nairobi,
lakini ilifanya maandalizi yake ikiwa na hali ngumu kutokana na kutopata sapoti
yoyote kama tulivyozoea katika timu za soka.
Kama hiyo
haitoshi, mpaka sasa hakuna kiongozi wala taasisi yoyote aliyejitokeza
kuendesha kampeni ya kuisaidia timu hiyo ambayo itaiwakilisha Tanzania katika
mashindanio ya dunia.
Lakini kila
mara tumekuwa tukishuhudia zikiundwa kamati mbalimbali za kuzisaidia timu za soka ambazo zinashiriki mashindano nje ya
nchi, lakini hatujawahi kusikia kuna kamati ya kusaidia timu ya riadha ishinde
au timu ya ndondi.
Kwa mfano
sasa hivi Serikali pamoja na Shirikishola Soka Tanzania (TFF) wameunda kamati
ya kuicchangia timu ya Taifa ya Vijana chini ya mkiaka 17 (Serengeti Boys)
inayoshiriki fainali zxa Mataifa ya Afrika (AFCON) mwezi Aprili kule Gabon.
Siyo mbaya
kwa kitu kama hicho kufanywa na serikali, lakini Serikali wadau inapaswa kutambua kuwa
Tanzania sio ya soka pekee kuna michezo kingine pia inahitaji kusapotiwa kwani
inaweza kuiletea sifa Taifa.
Ni jambo la
kusikitisha na kuvunja moyo kwa sababu michezo hiyo hiyo isiyothaminiwa ndiyo
inayoliletea sifa Tanzania katika medani ya kimataifa.
Nchi nyingi
zilizoendelea zinathaimini michezo yote na ndio maana zinafanya vema zaidi,
lakini sisi tunathamini soka tu kwa sababu unaonekana ndio unamaslahi ndani
yake.
Ifikie
mahala watanzania tubadilike kwa
kuachana na kasumba ya kuuthamini mpira wa miguu tu badala yake kutoa usawa kwa michezo mingine ili tuweze kupiga
hatua zaidi.