Na Dina Ismail
KADIRI miaka inavyosonga
ndivyo mwamko na chachu ya
kusaka mafanikio ya soka
yanavyoongezeka.
Hilo halina ubishi kwani tumeshuhudia mengi katika miaka ya karibuni na mojawapo ni kwa wachezaji wa Kitanzania kuitangaza nchi
katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla kupitia soka ya kulipwa.
Katika harakati hizo
za kusaka mafanikio, wiki iliyopita kumezalishwa makocha wapya 27 ambao walifuzu
kozi ya kati iliyoratibiwa kwa kufuata miongozo ya
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na lile la Afrika (CAF).
Kozi hiyo ambayo ilijazwa na idadi kubwa ya wachezaji mahiri waliokuwa wakizicheza timu kongwe za Simba na Yanga na
ile ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambapo siku
ya ufungaji mgeni rasmi alikuwa Rais wa
TFF, Jamal Malinzi.
Malinzi alifurahishwa na idadi kubwa ya makocha
waliohitimu na na kusema kuwa itasaidia
kukuza soka nchini , huku akisikitishwa na
ushiriki wa wanawake ambapo ni mmoja tu kati ya
27 aliyejitokeza na hivyo kutoa rai kwa wanawake kujitokeza kwenye kozi
za namna hiyo.
Kujitokeza kwa nyota hao wa zamani kushiriki kozi hiyo ni
jambo la kupongezwa kwani inaonesha
ni jinsi gani wana uchungu na maendeleo ya nchi yao hivyo wameona
kufanya hivyo kutasaidia kwa namna moja ama nyingine.
Ikumbukwe, wengi wa washiriki wa kozi hiyo walipata kutoa
mchango mkubwa katika soka Tanzania enzi za uchezaji wao hivyo naamini kupitia
mafunzo hayo pamoja na uzoefu walionao wa kisoka kutasaidia kupatikana kwa
wachezaji bora zaidi chini ya mikono yao.
Hata mwanamama pekee aliyeshiriki kozi hiyo, Doris Malyaga
ambaye ni mwandishi wa habari za michezo nchini, mbali na ukufunzi huo pia
ataitumia vema kalamu yake katika kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi
katika kozi kama hizo.
Hii in maana kwamba, kama kutakuwa na makocha wengi wanawake
wenye viwango na utaalamu wa hali ya juu
ni wazi kwamba itapunguza idadi ya makocha wa kiume katika timu za wanawake.
Hivyo basi mafunzo
waliyoyapata yasiishie kuwavimbisha vichwa, vyeti walivyoviopata visiwe mapambo
katika kuta za nyumba zao bali wayatumie kuwafunza wachezaji
wenzao na hasa timu za vijana ambazo ni muhimu sana katika mustakabali
wa matunda ya baadae.
Kama hiyo haitoshi, makocha hao wapya wasibwetye na kozi
hiyo hivyo wanawajibu wa kujingeza zaidi
ili kuweza kufikia katika madaraja ya juu
ili siku zijazo Tanzania itanue wigo wa kuwa na makocha wanaofundisha
nje ya Tanzania.
Baada ya hatua hiyo naamini kila mshiriki wa kozi hiyo
hatobweteka na hatua hiyo hivyo atakuwa na jukumu la kujiongeza zaidi ili
kupanda daraja.
Kozi hiyo iliendeshwa na
mkufunzi anayetambuliwa na CAF
Wilfred Kidao, akisaidiwa na kipa
mkongwe wa zamani Manyika Peter
aliyefundisha mtaala kwa makocha wa
makipa, Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyefundisha
kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka pamoja na mMkufunzi wa muda mrefu wa soka,
Hemed Mteza.
Mbali na Malyaga , washiriki wengine walohudhuria kozi hiyo ya siku 14 ni pamoja na Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule,
Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.
Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu,
Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud
Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said
Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.