YANGA Sc imetinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kuikwanyua Simba 1-0,mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa,Dar es Salaam.
Max Nzegeli ndiye aliyeipa ushindi Yanga mchezo huo ambapo uushindi wao utawakutanisha na Azam Fc katika fainali itakayopigwa Jumapili.
Simba ambayo imevuliwa ubingwa wa Ngao ya Jamii itacheza na Coastal Union ya Tanga katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Azam Sc imetinga fainali hiyo baada ya kuibanjua Coastal Union mabao 5-2katika nusu fainali iliyopigwa Visiwani ,Zanzibar