Na Dina
Ismail
WASANII maarufu nchini
wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali ‘King’ Kiba
wanatarajiwa kurekodi wimbo wa
pamoja ambao ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuichangia timu ya
Taifa ya Vijana wenye umei chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’.
Nyota hao
ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Serengeti Boys
wamekuwa na msigano mkubwa kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha
mgawanyiko mkubwa baina ya mashabiki wao.
Diamond na
Kiba wataungana na nyota wengine wa bongo fleva katika kuimba wimbo huo
wakiwemo Mwasiti Almasi, Darasa na
Vanesa Mdee ambapo tayari kila mmoja ameshapatiwa ala kwa ajili ya kuingiza
sauti.
Chanzo cha
kuwepo kwa ‘bifu’ kati yao mpaka sasa hakijajulikana, huku kila mmoja akikana kuwepo kwa hali hiyo lakini bado wameshindwa kufanya kazi pamoja kama
ilivyo kwa wasanii wengine.
Baadhi ya
wadau wa muziki wamejaribu kuwakutanisha pamoja wasanii hao ili kuondoa ‘bifu’ walilonao lakini imeshindikana, huku
tukishuhudia madongo ya kila mmoja akimrushia mwenzake katika mitandao ya
kijamii.
Hilo si
jambo zuri kwa wasanii wakubwa kama hawa ambao
kutokana na umahiri wao wamekuwa wakiipeperusha bendera ya Tanzania kila
mara katika medani ya kimataifa kwa
nyakati tofauti.
Kwa sasa
wasanii hao wanakutana katika kamati hiyo ya Serengeti Boys ambapo kwa namna moja ama nyingine
watahitaji kuwa na mawasiliano ili kuhakikisha wanatimiza wajibu ndani ya kamati hiyo ili kufanya mambo yaende
sawa.
Hivyo ni wakati wa nyota hao kuzizika rasmi tofauti zao kwa kufungua ukurasa mpya wa
kusaidiana na kushirikiana katika kazi zao na hivyo kusaidia maendeleo ya sanaa
ya Tanzania.
Itakuwa ni
jambo la jema tukisikia tamko toka kwao kama wameingia studio kurekodi kazi ya
pamoja, au mmoja wapo kamshirikisha mwingine katika moja ya kazi yake ama lebo
ya ya Diamond na lebo ya Kiba zinashirikiana katika kuinua wasanii chipukizi.
Diamond na
Kiba ni wasanii wenye vipaji vya hali ya juu hivyo naamini kama watakuwa na
ushirikiano ni wazi watapata mafanikio zaidi ya ilivyo sasa, kwa jinsi
wanavyokubalika pindi wakianza kuwa na uhusiano mzuri ni wazi wataliteka zaidi
soka la muziki.
Ni wasanii
ambao wametembea katika nchi nyingi duniania na hivyo kujifunza mengi mazuri
kupitia wasanii wakubwa waliokutana nao hivyo kama watamaliza tofauti zaom
wataweza kubadilishana uzoefu ili kuweza kujijenga zaidi kisanaa.
Hivyo
wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa na wasanii wengine na hasa chipukizi ambao mara
nyingi wanapenda kufuata nyayo za watu waliopata mafanikio katika kazi zao sasa
kama wanakuiwa na uhasama chipukizi watajifunza nini kutoka kwao?
Kwamba,
Diamond anazijua njia za magharibi na Kiba anazijua za Mashariki sasa wakiwa na
mahusiano mazuri ni wazi kila mmoja atamuonesha njia mwenzake watazidi
kujiongezea mashabiki na hatimaye kujiongezea vipato vyao kwani watapata fursa
za kutumbuiza maeneo mengi zaidi.
Kama
watamaliza tofauti zao pia itasaidia kuongeza mapato yao kupitia kazi zao kwani
hata wataungwa mkono na mashabiki wa kila upande ambao watanunua kazi zao na hatab kujitokeza
kwa wingi katika maonesho yao.
Kiba na
Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja
ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika zitakazopigwa nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.
Katibu wa
Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe wengine ni pamoja na Miss Tanzania 1999 ,
Hoyce Temu, Mtangazaji wa EFM Radio na TV, Maulid Kitenge, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel
Tanzania, Beatrice Singano, Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers
Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.