Na Dina Ismail
NAKUMBUKA zamani kulikuwa na michezo mingi sana ya watoto na
kila mida ya jioni na siku za mwisho wa juma
watoto walijikusanya katika maeneo ya wazi, pembezoni mwa nyumba au katika vibaraza kwa ajili ya kucheza.
Makusanyiko hayo ya watoto yalifanyika baada ya kumaliza
majukumu yao ya kishule au kwa wale waliokuwa wakisoma madrassa waliungana na
wenzao baada ya kurejea nyumbani.
Kuna michezo iliyohusu watoto wa kike pekee, watoto wa kiume pekee na kuna michezo ambayo
ilihusisha watoto wa jinsia zote.
Michezo kama mpira wa miguu, mdako, kombolela,
kujipikilisha, kuruka kamba, kibababa na kimamama, mstari kati, rede, bao,
kipande na mingineyo ndiyo ilishika kasi.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni utandawazi umeshika
kasi kwa watoto kupendelea zaidi
kuangalia ‘cartoon’ pindi warejeapo masshuleni ama ki[pindi cha likizo na
mapumziko ya mwisho wa wiki.
‘Cartoon’ zimeteka zaidi
akili za watoto wengi na hasa wa mijini
na hivyo kuwafanya washindwe hata kujihusisha na michezo mingine kama
ilivyo kuwa zamani sababu ya cartoon.
Mtoto akikanyaga tu ndani kabla hata hajavua nguo za shule
moja kwa moja ataenda washa TV na kuangalia mactaroon kwa dakika kadhaa kabla
ya kwenda kubadilisha na kuendelea na burudani yake hiyo.
Kama mzazi usipokuwa mkali mtoto atakaa kakodoa macho kwenye
tv mpaka usiku mkali bila hata ya kukumbuka kufanya vitu vingine ikiwemo kazi
za shule au kufanya maandalizi mengine
kwa ajili ya shule kesho.
Kwa jinsi watoto walivyotekwa
na Cartoon kuna baadhi huwapa mitihani wazazi wao pindi wanapowafanyia manunuzi
ya nguo, mabegi na vifaa vya shule
ambapo hutaka wanunuliwe vilivyo na picha za cartoon wanazozitaka wao;kinyume
na hapo hamtaelewana.
Yaani hata wakiwa mashuleni stori zao ni cartoon utasikia
sijui cartoon gani mpya imeingia, mara kituo hiki ndio kina carton nzuri,
mtoto anajua hadi ratiba za carton
katika vituo vya tv kulikio hata ratiba za masomo shule.
Lakini ukija mwenye michezo,, mtoto hajua hata mchezo mmoja
na hata ukijaribu kumuuliza unapenda mchezo hani hana cha kujibu, uliza cartoon
sasa utaorodheshwa mpaka uchoke na roho yako.
Sio kwamba cartoon hazifai kwa watoto wetu la hasha ila
ziangaliwe kwa muda stahiki kwani zipo cartoon ambazo zina mafunzo mazuri tu
kwa watoto, zipo zinazoburudisha.Pia husaidia kuwafunza kujua lugha hasa ya
kiingereza kwa ufasaha.
Kwa hali ilivyo, wazazi hawana budi kusiamama kidete
kukabiliana na hali hii ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika mstari
ulioonyooka kwa kufanya vitu kwa kuendana na ratiba.
Kuna methali isemayo,
Samaki mkunje angali mbichi:hivyo ni vema wazazi kusimamia watoto ili kuwarejesha
katika kujifunza michezo na masuala
mengine kwa manufaa ya baadaye.
Kwamba, watoto wasimamiwe kuhakikisha wanakuwa na muda maalum
wa kucheza, kufanya kazi za shule na pia kujifunza kazi nyingine ndogo ndogo za
nyumbani bila kuangalia jinsia.
Bila kufanya hivyo tutajikuta tunakosa wanamichezo au ‘watu
flan’ wa baadaye kwani bila ya kuanza kujifunza kitu au kuwa na mapenzi nacho
tangu utotoni ni vigumu kukifanya ukubwani tena kwa mafanikio.
Wazazi tusaidie walimu katika kusiamamia watoto wetu na
tusiwarudishe nyuma walimu kwani kama shule wamefunzwa kitu ni vema na nyumbani wakaelekezwa kidogo, kutiwa moyo
au kuongezewa kiasi ili kumsaidia mtoto.