Na
Dina Ismail
HIVI
karibuni msanii wa muziki kipya nchini
Emmanuel Elibariki maarufu kama
‘Na alitoa wimbo uitwao ‘Wapo’
ambao ulikuwa na mashairi makali kiasi
cha kupelekea Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuufungia.
Awali
msanii huyo alikamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kutokana na mashairi
yaliyopo katika wimbo huo ambayo yanadaiwa kuwasema viongozi wa Serikali, kabla
ya Waziri wa Habari Utamaduni, sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutaka
achiwe huru.
Pia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli naye akitoa zuio la
wimbo huo huku akimshauri auboreshe kwa
kuongeza baadhi ya vipengele kadhaa ikiwemo
vinazozungumzia Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na
watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.
Nay
msanii anayeimba muziki wake kwa mtindo wa Hip Hop amekuwa akikumbana na
vifungo vya Basata mara kwa mara sambamba na kupewa onyo kutokana na nyimbo
zake kukukiuka maadili ya Kitanzania.
Mara
kwa mara Basata imekuwa ikiwakumbusha wasanii na wadau wa kazi kuzingatia
maadili ya nchi sambamba na kufanya ubunifu wa hali ya juu kwa kutunga nyimbo
zinazofikisha ujumbe kwa kufundisha , kuburudisha, kuelimisha na kuona.
Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha sheria ya
BASATA namba 23 ya mwaka 1984, baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za
sanaa na mamlaka kuhakikisha yote yanayofanyika katika sanaa hayaachi taifa na
wasanii katika hali zisizo salama.
Hii ni mara
ya tatu kwa Basata kuzifungia nyimbo za Nay kutokana na kukiuka maadili, ambapo
kwa nyakati tofauti lilipata kuzifungia nyimbo zake zilizokwenda kwa jina
‘Shika Adabu Yako’ na ‘Pale Kati Patamu’.
Nay ni
msanii mzuri sana, mwenye kujiamini na
mwenye kipaji cha hali ya juu, lakini kinachomuangusha ni matumizi ya lugha
kali anazozitumia katika tungo zake ambazo mara nyingi zinaonekana
kuwadhalilisha baadhi ya watu.
Hana woga,
kwani kuna nyingine anafikia hatua hata ya kuwataja majina kabisa watu na hasa
wasanii maarufu ambao wanafanya ndivyo sivyo katika jamii.Anafanya hivyo kwa
lengo la kuwarekebisha.
Ni msanii
muwazi kwani hata nyimbo alizoshiruikishwa nyingi amekuwa akitirika mashairi ya
kupinga kitu flani ambayo ukiangalia kwa namna moja ama nyingine yanamaudhui
mazuri tu.
Wengi
hawamuelewi Nay na kumuona kama msanii mtukutu kitu ambacho sicho kwani Nay ni
msanii anayependa mambo yaliyonyooka, yani hapendi ubabaishaji hivyo kuamua
‘kumwaga radhi’.
Pia nyota
huyo, mara nyingi anapenda kutunga nyimbo kutokana na matukio ambayo yanakuwa
yanatamba kwa kipindi hiko na hivyo akitoa wimbo mara nyingi unapokelewa kwa
haraka sana na hivyo kuzidi kumuongezea umaarufu.
Ingawa kwa upande mwingine Nay anatumia vibaya kipaji
chake kwani kuna vitu vingine ni utashi wa mtu binafsi hivyo si vyema kumsema
katika wimbo kwa madai kuwa unamuweka
sawa.
Ili
kuepukana na utata kama wa Nay na
wasanii wengine wanaotoa kazi zisizo na maadili, ifikie wakati Basata
ikarekebisha kanuni na sheria zake
katika kusimamia sheria na maadili ya nchini kwa kuweka muongozo mkali kwa
wasanii wote iwe wa filamu au muziki.
Kwamba,
ingeweka sheria kwa watayarishaji wote wa muziki na filamu kutokabidhi kazi za
wasanii wanazozitayarisha mpaka zipitie Basata kwa ajili ya ukaguzi na ndipo
wawakabidhi wasanii wenyewe na kuanza kuzitangaza katika vyombo vya habari.
Kama hiyo
haitoshi, ingewetunga sheria kali ya kudhibiti hilo ili kulinda madili ya
nchi na kwa wale watakaokiuka sheria
haina budi kuchukua mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine.
Nasema hivyo
kwa sababu kuzuia wimbo ambao unakuwa umeshasambaa katika vyombo vya habari
hakusaidii lolote, hivyo ni vyema udhibiti ungeanzia kwa watayarishaji ili iwe rahisi kuwabana.
Pia Basata
inawajibika kutoa semina za mara kwa mara kwa wasanii ili kuweza kuwakumbusha
sheria, kanuni na maadili yanayopaswa kuzingatiwa wanapotayarisha kazi zao.