Na Dina
Ismail
WIKI iliyopita tumeshudia kutolewa kwa ratiba ya makundi ya kufuzu fainali za kombe la Mataifa
zitakazopigwa nchini Cameroon mwaka 2019, huku Tanzania ikipangwa kundi L pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho .
Katika droo iliyofanyika
mjini Libvreville, Gabon, michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo kwa mechi kuchezwa kati ya Machi 20 na 28 huku mechi za kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na
13, za pili Machi 19 na 27 2018, za tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8
na 16, 2018 na za tano Novemba 5 na 13, 2018.
Katika
michuano hiyo, raundi ya awali itazihusisha
timu za Comoros, Djibouti, Madagascar, Mauritius, Sao Tome E Principe na Sudan
Kusini.
Kundi L ukiliangalia kwa haraka haraka linaonekana ni
kundi rahisi zaidi kwa Taifa Stars, kwani
wapinzani wake wote
ni timu ambazo zipo ndani ya uwezo wake.
Kenya pia
itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na
Serra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika
ya Kati (CAR).
Mshindi wa
kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu
zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama
washindi wa pili bora.
Timu
zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye makundi A, B na C kukamilisha
idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu za Senegal, Equatorial Guinea na
Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco na Malawi na C kuna Mali, Gabon n
Burundi.
Makundi
mengine ni; D: Algeria, Togo, Benin na Gambia, E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya
na Shelisheli, G: DRC, Kongo, Zimbabwe na Liberia, I: Burkina Faso, Angola,
Botswana na Mauritania, J: Tunisia, Misri, Niger na Swaziland, K: Zambia,
Msumbiji, Guinea-Bissau na Namibia.
Cameroon
ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja na kama itashika nafasi
ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu
Hata hivyo
ukiangalia kiundani zaidi Taifa Stars hawapaswi kulidharau kwani mdharau mwiba
mguu huota tende hivyo haina budi kujipanga kama inacheza na timu yoyote kubwa.
Kwamba mara
nyingi mechi ambazo zinaonekana nyepesi ndio huwa ngumu zaidi kwa vile timu
pinzani inakuwa imejiandaa kikamilifu, hivyo kama Stars itaamua kubeteka na
kufanya maandalizi ya zimamoto itakula kwetu!
Tayari
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ilishatangaza Mzalendo, Salum Mayanja kuwa kocha mkuu wa
muda wa Taifa Stars, akirithi mikoba ya mzalendo mwenzake Charles
Boniface Mkwasa.
Hivyo basi
Mayanja atakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha anateua kikosi bora zaidi ambacho
kitaweza kufannya vema sio tu kwa Afcon, bali kwa michuano mingine
itakayoshiriki akiwa kama kocha mkuu.
Kama hiyo
haitoshi umoja na mshikamano baina ya wachezaji, benchi ka ufundi na viongozi
wa TFF vyote vinahitajika ili
kuhakikisha timu inakuwa katika ubora wa hali ya juu na hivyo kusaidia
kuipatikanan kwa uishindi mnono na hatimaye kutinga fainali.
Katika
kuelekea fainali za mwaka huu nchini Gabon, Stars iliiashia hatua ya makundi baada
ya kushika mkia katika Kundi G lililokwa
na timu za Nigeria na Misri.
MAKUNDI KWA UKAMILIFU KUFUZU AFCON
2019
A: Senegal,
Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar
B: Cameroon,
Morocco, Malawi, Comoros/Mauritius
C: Mali,
Gabon, Burundi, Djibouti/Sudan Kusini
D: Algeria,
Togo, Benin, The Gambia
E: Nigeria,
Afrika Kusini, Libya, Shelisheli
F: Ghana,
Ethiopia, Sierra Leone, Kenya
G: DRC,
Kongo, Zimbabwe, Liberia
H: Ivory
Coast, Guinea, Afrika ya Kati, Rwanda
I: Burkina
Faso, Angola, Botswana, Mauritania
J: Tunisia,
Misri, Niger, Swaziland
K: Zambia,
Msumbiji, Guinea-Bissau, Namibia
L: Cape
Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho