Arsenal
imejiongezea matumaini ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya
England, licha ya kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Stoke.
The
Gunners walinyimwa ushindi na Peter Crouch aliyefunga bao dakika ya tisa
akiunganisha kwa kichwa krosi ya Matthew Etherington.
Wageni
walisawazisha haraka tu kupitia kwa Robin van Persie aliyeunganisha pasi ya
Tomas Rosicky.
Arsenal
imejiimarisha nafasi ya tatu ikifikisha pointi 66, baada ya kucheza mechi
36.
Katika mchezo mwingine Nikica Jelavic alifunga mabao mawili
wakati Everton ikikaribia kumaliza juu ya Liverpool baada ya kuifunga Fulham 4-0
kwenye Uwanja wa Goodison Park.
mshambuliaji
huyo wa Croatia alifunga mawili kabla ya mapumziko, huku Marouane Fellaini
akifunga lingine na Tim Cahill
akifunga la nne.
Ushindi
huo unaipeleka Everton nafasi ya saba, wakiwazidi wapinzani wao wa Merseyside
pointi tano.
Ni Stoke sio Everton !!!
ReplyDelete