LIGI Daraja la Kwanza Tanzania
Bara, inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo kati ya Mgambo Shooting ya Tanga na
Polisi Tabora Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mgambo ndio inaoongoza ligi hiyo
kwa pointi zake 11 wakati Polisi Tabora ina pointi nne. Mechi ya pili itakuwa
kati ya Polisi Morogoro yenye pointi kumi na Polisi Dar es Salaam yenye pointi
sita.
Mechi ya pili itakuwa kati ya
Polisi Morogoro yenye pointi kumi na Polisi Dar es Salaam yenye pointi sita.
Jana Tanzania Prisons ya Mbeya
na Mlale JKT ya Ruvuma zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa fainali za
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) uliochezwa leo (Aprili 14 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Jamhuri, mjini hapa.
Kwa sare hiyo Tanzania Prisons
imefikisha pointi nane wakati Mlale JKT inazo tano. Timu tatu za kwanza katika
fainali hiyo ya 9 bora zitapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao.
Mlale JKT ndiyo walioanza
kufunga dakika ya 61 kwa mpira wa adhabu uliopigwa nje ya eneo la hatari na
mshambuliaji Edward Malimi katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Shabani
Shata kutoka Kigoma.
Dakika sita kabla ya filimbi ya
mwisho beki Richard Mwakalinga aliisawazishia Tanzania Prisons inayofundishwa
na Stephen Matata baada ya kufanya shambulizi kubwa langoni mwa Mlale JKT.
Hadi tuna kwenda mitamboni,
mechi ya pili kati ya Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City ya Mbeya ilikuwa
ikiendelea huku Rhino Rangers ikiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 18
na kiungo Salum Tabayi.