ALLY KAMWE AJITOA YANGA SC



Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ametangaza kujiondoa kwenye nafasi hiyo baada ya kuhudumu kwa misimu miwili tangu Septemba 25, 2022.

"Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua wakati sahihi wa kuondoka jukwaani. Kwa hekima hii, nawaambia kuwa ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka jukwaani. 

"Nimesimama kwa miaka miwili juu ya hili jukwaa, tumeimba, tumecheza, tumefurahi, na tumeshinda pamoja. Muda wangu umemalizika, asanteni sana.

"Tutaonana tena nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha juu ya jukwaa." Ameandika Ally Kamwe

Post a Comment

Previous Post Next Post