Acer e10 Series kuwarahisishia kazi wafanyabiashara


 Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Sixunited   imezindua vishkwambi maalum 'Acer e10 Series Notebook' kwa ajili ya kuwarahisishia  wafanyabiashara  katika utendaji wao.

Uzinduzi wa bidhaa hiyo umefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau pamoja na wafanyabiashara mbalilmbali.

Meneja wa kampuni hiyo, hapa nchini Theresia Mwita alisema wamefanya hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa teknolojia hiyo.

Alisema hatua hiyo pia itasaidia kupatikana kwa ajira kwa vijana kupitia bidhaa hiyo itakayouzwa kwa gharama nafuu.

"Tumelenga kurahusisha upatikanaji wa teknolojia iliyo bora na kwa gharama nafuu,nitoe wito kwa  wafanyabiashara kuhakikisha hawakosi kifaa hiki ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwao,"Alisema Theresia

Post a Comment

Previous Post Next Post