TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo imelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia katika mchezo wa Kundi F kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Stars ilitangulia kupata bao hiko kupitia shuti kali la Simon Msuva katika dakika ya 11 bao ambalo lilizipeleka mapumziko timu hizo kwa Stars kuingoza 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari kubwa kabla ya Patson Daka kusawazisha katika 88 kwa mpira wa kichwa.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Tanzaia kuendelea kushika mkia katika kundi F kwa kuwa na pointi moja ambapo Morocco inaongoza ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa Zambia (2) na DR Congo (2).
Michezo iliyosalia itapigwa keshokutwa Jumatano Januari 24, 2024 ambapo Tanzania itakipiga na DR Congo na Zambia itakwaana na Morocco
Tags
SPORTS