KAMPUNI ya Usafirishaji wa Vifurushi ya DHL, imesema ujio wa
Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu England
linaloshikiliwa na Mashetani Wekundu, Manchester
United ya Uingereza jijini Dar es
Salaam hivi karibuni umeleta faraja kwao na Watanzania
kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Maneja wa Kampuni hiyo
nchini, Blaise De Souza, alisema, ziara hiyo imetoa fursa kwa Wananchi na
wapenda soka kulishuhudia.
“Kuja kwa kombe hilo ,
kumetoa fursa kwetu na imeonyesha kwa jinsi gani tunafanya kazi kubwa kwa
wateja wetu,” alisema.
Alisema, pia imetuo fursa kwa wafanyakazi wao kukutana ana
kwa ana na baadhi ya nyota wa zamani wa Man U, wakiwemo Quinton Fortune na Gary
Bauley.
Aidha alisema, DHL imefanya kazi kubwa kulileta kombe hilo na kutoa fursa kwa
Watanzania kulioana na kupiga picha nalo.