SIKU chache baada ya kuwepo kwa utata juu ya ujio wa
klabu yaTp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya
kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya Simba, uongozi wa Simba umewatoa hofu
mashabiki wa Simba na wa soka kwa ujumla juu ya ujio huo.
Hivi karibuni aliyewahi kuwa mdhamini wa Simba na Makamu
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Azim Dewji alitangaza kuileta Tp
Mazembe kwa ajili ya kuipa makali Simba ambayo inatarajiwa kucheza mechi ya
kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage ameiambia mamapipiro blog kuwa
yeyue na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Azim Dewji wamekuwa
wakifanya mawasiliano ya mara kwa mara na mmliki wa TP Mazembe Mose Katumbi.
Alisema anashangazwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya
vyombo vya habari zikimnukuu kocha msaidizi wa Tp Mazembe Lamine Ndiaye kutokuwa na taarifa za ziara hiyo kitu ambacho
hakina mantiki yoyote kwa kuwa kocha kazi yake ni kufundisha tu.
“Kama mtu anataka uhakika awasiliane na Katumbi ama
katibu wake Kitenge, sisi tunafanya mazungumzo wenyewe kwa wenyewe (viongozi)
na mambo yakiwa tayari wanapewa taarifa wengine ndiyo maana hata baadhi ya
viongozi wenzangu wea Simba hawana taarifa rasmi,”Alisema Rage.
Rage aliongeza kuwa mipango kuhusiana na ujio wa timu
hiyo ambayo nayo inatarajiwa kukwaana na El Mereikh ya Sudan katika Ligi Ya
mabingwa barani Afrika yanakwenda vema na kama kutakuwa na mabadiliko yoyote
watatoa taarifa rasmi.Katika hatua nyingine, Rage amempongeza Dewji kwa
kutimiza ahadi yake ya kuwakabidhi wachezaji wa timu hiyo kitita cha shilingi
milioni 15 baada ya kuitoa Es Setif ya Algeria na kutinga hatua ya 16 bora ya
michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).