Mzee Chakupewa akizungumza na wanahabari kuhusiana na tafrani hiyo.
Mchana wa leo almanusura mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa katika klabu ya Yanga usifanyike baada ya baadhi ya wanachama maarufu kama Makomandoo kuanzisha vurugu wakitaka mtangazaji wa
kituo cha redio Clouds, Alex Luambano aondolewe kwenye chumba cha mikutano
klabu hapo.
Wanachama
hao walidai kuwa wamekuwa wakikerwa na watangazaji wa michezo wa kampuni hiyo
ambao wamekuwa wakiitangaza vibaya klabu hiyo hivyo hakuna sababu ya kuwepo
hapo.
"Toka nje nenda huko mkalipwe mshahara na klabu ya ... hapa hatuwataki na wenzako kina...walidai huku wakiwataja badhi ya watangazaji wa kituo hicho.
Kutokana na hali hiyo kuchafuka ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alimtaka Luambano kutoka ili kuepusha shari lakini wanahabari walipinga hilo na kusema kama atatolewa hawatakuwa tayari kusikiliza walichoitiwa.
Hata hivyo
busara zilitumika kuwatuliza wanachama hao ambapo mmoja wao Mzee Bilali Hemed ‘Chakupewa’
aliweza kutuliza purukushani hizo na ndipo Sendeu alianza kuzungumzia kilichomfanya aitishe mkutano huo.