KOCHA Sir Alex Ferguson amemtetea Federico Macheda kwamba
ataibuka tena katika kipindi cha kucheza kwake kwa mkopo na kurejea kufanya
vitu Manchester United.
Mshambuliaji huyo Italia hakuwa na furaha akiichezea
Sampdoria msimu uliopita na alipotua QPR, baada ya kuondoka kwa kocha Neil
Warnock na Mark Hughes kuchukua nafasi, alisajili wachezaji wenye majina
makubwa kama Djibril Cisse na Bobby Zamora Januari.
Hiyo ilitokana na matatizo ya kifundo cha mguu yaliyomuandama
Macheda na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza Loftus Road hadi akarejea Manchester
wiki iliyopita kwa matibabu.
Bado kocha Ferguson ana matumaini na kijana huyo mwenye umri
wa miaka 20 na anaamini jinamizi la majeruhi linalomuandama hivi sasa litafika
mwisho na ataanza kung’ara tena.