Ligi Kuu ya Vodacom imeingia raundi ya 25
ambapo kesho (Aprili 25 mwaka huu) Oljoro JKT itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Raundi hiyo itakamilika kwa mechi nne;
Aprili 28 mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye
Uwanja wa Chamazi.
Azam na Toto African
zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad
itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo itafunga msimu wa
2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga
(Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid,
Arusha) na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi nyingine zitakuwa kati
ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu
(Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro
United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).