Mel B |
NYOTA wa lililokuwa kundi la Spice Girl, Mel B amesema
anataka kubadili uraia na kuwa Muastralia.
Muingereza Mel, mwenye umri wa miaka 36, hivi karibuni
amekuwa akifanya kazi zake katika Majiji ya London, LA na Sydney.
Ni maarufu Australia akiwa amewahi kuwa jaji wa shindano la
X Factor na hivi karibuni atashiriki katika mchezo wa Dancing With The Stars.
Mke huyo wa mtu na mama wa watoto watatu alisema: "Ningependa
kuwa raia wa Australia." Motto wake mkubwa Phoenix mwenye umri wa mikaka
13, anasoma Sydney.
Mel alisema: "Nimefungua duka hapa. Tuna furaha na
tumejipanga,”.