TIMU ya soka ya taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 ' Ngorongoro Heroes' imeanza leo vema mechi yake ya kwanza ya raundi ya awali kuwania kufuzu
fainali za Afrika vijana wa umri huo, baada ya kuwafunga wenzao wa Sudan kwa
mabao 3-1.
Mshambuliaji wa timu hiyo anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Tp Mazembe ya Jamhuri yua Kidemokrasia ya Congo (DRC) Thomas Ulimwengu aliifungia
Ngorongoro Heroes bao la kwanza, kabla ya Ramadhani Singano kufunga la pili dakika na la tatu likipachikwa na Simon Msuva.