Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kinaendelea tena leo kwa mechi tano zitakazochezwa kwenye miji ya Bukoba, Mwanza, Dar es Salaam,
Mlandizi na Dodoma.
Mabingwa watetezi Yanga
watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba wakati
Toto Africans itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Vinara wa ligi hiyo Simba
wataoneshana kazi na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Ruvu
Shooting na Moro United zitaumana kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Nayo
Polisi Dodoma itakuwa mwenyeji wa Coastal Union mjini Dodoma.