KATIKA
hali ya kushangaza, timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro
Heroes, juzi ilizuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .
Katika
kile kilichoonekana ni mipango mibovu ya watendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ,
(TFF), timu hiyo ilifika uwanjani hapo ikiwa na Kocha wake, Mdenish, Kim
Poulsen, lakini katika mazingira ya kutatanisha, walinzi wa uwanja huo waligoma
kufungua milango ili gari la timu hiyo liingie.
Kutokana
na hali hiyo, Kocha Poulsen, alionekana akiwasiliana na viongozi wa TFF, lakini
mara ghafla alikata simu na kuamuru msafara wa timu yake ugeuze na kuondoka
eneo hilo .
Alipoulizwa
kiongozi mmojawapo wa TFF kuhusiana na tukio hilo , alielezea kushangazwa na hatua hiyo na
kubainisha kuwa timu hiyo ni ya taifa hivyo haikupaswa kuzuiliwa kuingia
kufanya mazoezi.