Na
Ezekiel Kamwaga, Setif
KIKOSI
kamili cha Simba kimewasili jijini Setif leo majira ya saa saba na nusu mchana
saa za hapa (saa tisa na nusu saa za huko), baada ya safari ndefu ya kutoka Algiers .
Simba
iliwasili Algeria
jana lakini ilishindwa kwenda Setif kutokana na kukosa usafiri wa ndege, na
kukataa usafiri wa basi ulioandaliwa na wenyeji wao.
Wakati
wenyeji wakidai kwamba usafiri wa kutoka Algiers ilikolala Simba hadi Setif ni
masaa matatu, leo Simba imetumia takribani dakika 45 kwenda mji wa Bizaya
(Bezaia) kwa usafiri wa anga na kisha kupanda basi kwa muda wa karibu masaa
mawili na nusu hadi kufika Setif.
Kwa
kawaida, usafiri wa ndege nchini Tanzania
muda wa dakika 45 hutosha kumfikisha mtu mkoani Arusha kwa usafiri wa anga
akitokea Dar es Salaam
na hivyo viongozi wa Setif walikuwa wakisema uongo walipodai kuwa safari ya
basi ingetumia muda wa masaa matatu.
Kama
Simba ingefuata ushauri wa Setif jana, ni wazi kuwa ingeingia katika mji huu
usiku na isingeweza kufanya mazoezi siku ya jana.
Hata
hivyo, msafara wa Simba chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage, ulisimama kidete
na kuamua kulala Algiers
jambo lililosaidia timu kufanya mazoezi jana.
Wekundu
wa Msimbazi wamefikia katika Hoteli ya Zidane iliyopo katikati ya mji wa Setif
na kuna taarifa kuwa hoteli hiyo ni miongoni mwa vitega uchumi vya mwanasoka
bora wa zamani wa dunia, Zinedine Zidane, Mfaransa mwenye asili ya Algeria .
Jana
Simba ilifanya mazoezi yake katika uwanja wa kijeshi jijini Algiers chini ya ulinzi mkali kwa muda wa
masaa mawili.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka katika benchi la ufundi la Simba leo klabu itafanya
mazoezi yake katika Uwanja wa Mei 8, 1945 majira ya saa 12 jioni kwa saa za
hapa.
Uwanja
huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi ya Kombe la CAF baina ya Simba na
Setif iliyopangwa kufanyika keshokutwa saa 12 jioni kwa saa za hapa sawa na saa
mbili usiku kwa saa za Tanzania .
Msafara
wa Simba umekuwa kivutio kikubwa nchini Algeria , kutokana na unadhifu wa
wachezaji wake ambao wote wamevaa suti za wabunifu zinazowatofautisha na abiria
wote wengine kwenye viwanja vya ndege ambako timu imepita.
Kwa
mujibu wa Shirikisho la Soka la Algeria ,
mechi ya keshokutwa itachezeshwa na waamuzi kutoka Tunisia
huku Kamisaa wa mchezo akiwa anatokana nchini Gabon .
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete