Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
limewateua waamuzi wane wa Tanzania kuchezesha mechi ya marudiano ya 16 bora ya
Kombe la Shirikisho kati ya Black Leopards ya Afrika Kusini na Warri Wolves ya
Nigeria itakayochezwa nchini Afrika Kusini kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka
huu.
Waamuzi hao ni Waziri Sheha
atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa John Kanyenye na Erasmo
Jesse. Mwamuzi wa akiba (fourth official) atakuwa Israel Mujuni. Kamishna wa
mechi hiyo atakuwa Aurelio Mathias wa Msumbiji.
Mechi ya kwanza kati ya timu
hizo itachezwa Jumapili (Aprili 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Warri City ulioko
Jimbo la Delta nchini Nigeria na itachezeshwa na waamuzi kutoka Senegal wakati
Kamishna atakuwa Inyangi Bokinda wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC).