Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 40,980,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo
kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki
9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda
kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa
tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh.
2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina-
Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh.
4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).