Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia
wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi
wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa
kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa
na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe
kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.
Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema
hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta
taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza
mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua
huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone
imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii
zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na
Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki.
Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama
kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia kupata huduma. Watanzania
tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia
kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.
Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo
tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana
Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua
hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye
mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye
Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua
browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na
nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.
Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na
Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba
255779477477 ili uweze kuunganishwa.