Washiriki Miss Tabata katika pozi
Na Mwandishi Wetu
Shindano la kusaka Miss
Tabata 2012 linafanyika kesho katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo
Joseph Kapinga amesema leo kuwa bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa
zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo.
Mratibu wa shindano hilo
lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh
500,000/- na king’amuzi ambayo imelipia miezi sita yenye thamani ya sh 800,000
iliyotolewa na Multichoice.
Mshindi wa pili atapata sh
500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja
atapata sh 200,000.
Kapinga alisema warembo
watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala.
Warembo wengine watakaoingia
10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila
moja.
Kapinga alisema shindano hilo
pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano
la Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu sio la
kukosa kwani litakuwa ni la aina yake ukizingatia kuwa litatumika kusherekea
miaka 10 tangua kuanza kuandaa Miss Tabata,” alisema Kapinga.
Alisema warembo waliyowahi
kushinda mataji mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka
10 ya Miss Tabata.
Shindano hili limedhaminiwa
na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito Entertainment,
Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In
Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.
Mrembo anayeshikilia taji la
Tabata kwa sasa ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa
wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata
Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha
Redds.
Katika shindano la mwaka juzi
Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia
taji la dunia la Miss Progressive International.