MWENYEKITI wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amefuta
uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya
ujumbe katika kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la
Soka Tanzania
(TFF).
Rage alitangaza
kujuzulu nafasi hiyo hivi karibuni kwa madai kwamba kamati hiyo imeshindwa
kusimamia sheria na kanuni za uendeshaji wa soka zinavyoeleza,kabla ya
kuwasilisha barua yake kwa Rais wa TFF, Leodger Tenga.
Rage amefuata uamuzi wake baada ya
kukutana na Tenga na kuzungumzia mustakabali mzima wa jambo hilo na kumtaka aendelee kuwepo.