TASWA imepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kiungo wa timu ya Simba ya Dar es Salaam
na mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mutesa Mafisango
kilichotokea alfajiri ya Alhamisi kwa ajali ya gari jijini Dar es
Salaam.
TASWA inatoa pole
kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, wachezaji wa timu hiyo, mashabiki na
Watanzania kwa ujumla kutokana na msiba huo mkubwa kwa familia ya mpira wa
miguu.
Tunaamini
waandishi wa habari za michezo wameguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo, kwani
wakati wa uhai wake marehemu alikuwa na ushirikiano mkubwa na wanahabari na
hakuwa mtu mwenye maringo, kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano kwa
wenzake.
Tunasema kifo
chake ni pigo si kwa Simba na familia yake tu, bali hata kwa timu ya Taifa ya
Rwanda na Wanyarwanda wote, ambao pia tunawapa pole kwa msiba huo.
Tunawapa pole
wanamichezo wote na kuwaomba wawe na subira na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu, huku wakiamini waandishi wa habari za michezo tupo nao pamoja katika
majonzi hayo na kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peoni.
Amina.
Kifo cha Mzee
Limonga
Tunapenda
kuwajulisha waandishi wa habari za michezo wote pamoja na wadau wengine kuwa
mtangazaji wa habari za michezo wa Redio Uhuru, Limonga Justine, amefiwa na baba
yake mzazi jana Alhamisi asubuhi kwenye hospitali ya Temeke, Dar es Salaam
.
Msiba upo Mbagala
kwa Mangaya, Dar es Salaam na maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Naomba tuungane naye mwenzetu katika kipindi hiki kigumu kwake na tumfariji kwa
kadri tuwezavyo kwa kuondokewa na mzazi wake. Nambari yake ya simu ni
0713-604578.
Nawasilisha.
Amir
Mhando
Katibu Mkuu
TASWA
18/05/2012.
0713-415346
KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NAPENDA KUTOWA
SALAMU ZANGU ZA RAMBIRAMBI NA KUWAPA POLE VIONGOZI WOTE ,WANACHAMA WOTE NA
WAPENZI WOTE WA SIMBA SPORTS CLUB YA JIJINI DSM ,KWA MSIBA MKUBWA SANA
ULIOWAPATA KWA KUONDOKEWA UHAI KWA MCHEZAJI WAO MAARUFU -PATRIC
MAFISANGO.
SISI VIONGOZI WA
TPBO PAMOJA NA KUWA NI VIONGOZI WA MCHEZO WA NGUMI LKN PIA HUPENDELEA SANA
KUHUDHURIA KUANGALIA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU ,KWANI NI MOJA A BURUDANI
TUIPENDAYO PIA,.
HIVYO BASI
TUNATAMBUWA SANA NA KUHESHIMU MCHANGO MKUBWA SANA AMBAO MAREHEMU PATRIC
MMAFISANGO ALIUTOWA KWA TIMU YA SIMBA PAMOJA NA WATANZANIA KWA UJUMLA HASA
VIJANA WADOGO WAPENDAO KUCHEZA MPIRA WA MIGUU-MAFISANGO ALIKUWA NI KIGEZO
KWAO.
MMI BINAFSI WAKATI
NIKIHUDHURIA MICHEZO MBALIAMBALI ILIYOKUWA IKCHEZWA NA KLABU YA SIMBA
NILISHUHUDIA MCHANGO MKUBWA ALIOKUWA AKIJITOLEA UWANJANI NA KUIFANYA SIMBA
SPORTS CLUB KUWA MSHINDI ,NA HATIMAYE KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA VODA-COM
MWAKA HUU..
TPBO INAPENDA KUWAFARIJI WACHEZAJ WOTE WA
SIMBA SPORTS CLUB KWA MSIBA HUO ,PAMOJA NA KWAMBA ITAWACHUKUWA MUDA MREFU SANA
KUSAHAU KIFO CHA MAFISANGO ,NINAWAOMBEA KWA MUNGU ILI AWAPUNGZIE MAJONZI NA
WALIONE HILI NI JAMBO LILILOPANGWA NA YEYE MWENYEZI MUNGU MUUMBA WETU ,PIA
WAZIDISHE KUMUOMBEA MUNGU ILI AMSAMEHE MAKOSA YAKE NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI
-AMEIN
NA NJIA NYINGINE
YA KUMUENZI MCHEZAJI MWENZAO NI KUHESHIMU KAZI YAKE YA UWANJANI, NA WAIGE
ALIVYOKUWA AKIJTUMA AWAPO UWANJANI, NA NIDHAMU YAKE ALIPOKUWA UWANJANI,. KWA
KUTENDA HAYO WATAKUWA WANAMUENZI VYEMA.
BWANA AMETOWA ,NA
BWANA AMETWAA- NENO LA BWANA LIHIMIDIWE-
EEH BWANA UMPE
RAHA YA MILELE PATRIC MAFISANGO NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE ,NA ASTAREHE KWA
AMANI.AMEEN
YASSIN ABDALLAH
MWAIPAYA -USTAADH
RAIS-TPBO