At akifanya mambo na wanenguaji wake
Barnbaba Boy naye hakupitwa
Ben Pol
Diamond Platnumz
Ommy Dimpoz kwa pozi
WASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Diamond, Roma, Isha Mashauzi, AT,
Barnaba, Omy Dimpoz, Ben Paul wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili
Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa Kirumba jijini
Mwanza, na kutoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa burudani ya Musiki wa
jiji hilo na vitongoji vyake.
Show hiyo kali iliyoanza majira ya saa 8 mchana ikitanguliwa na makundi
kadhaa ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva wa Jijini Mwanza ilizidi kupamba
moto muda hadi muda hadi pale wasanii Nguli na washindi wa Tuzo za Kili
Music Award 2012 walkipowasili uwanjani hapo.
Katika kukuza vipaji na kuibua vipaji vipya vya wasanii chipikizi Msanii
Christian Joachim maarufu kama Christian JJ alifanikiwa kuwashinda wenzake
wawili akiwepo mwana dada kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha
Jijini Mwanza Bertha Denis.
Christian JJ aliibuka kidedea baada ya kupata kura nyingi za mayowe zilizo
lipuka kutoka kwa mashabiki takribani wote uwanjani hapo na kuungana na
mshindi mwingine kutoka mkoani Dodoma ambao wataenda jijini Dar es Salaam
kurekodi nyimbo yao moja kwa Mtayarishaji wa Muziki maarufu.
Alianza jukwaani kupanda mwanadada wa Kikurya anaeimba Taarabu, Isha
Mashauzi wa Mashauzi Clasic ambaye alijinyakulia Tuzo ya Wimbo bora wa
taarabu kupitia wimbo wa Nani kama Mama na kukonga nyoyo za wapenzi wa
taarabu vilivyo kwa kuimba vibao vyake kadhaa.
Isha Mashauzi alifuatiwa Jukwaani na mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number
Oneambapo nae alishambulia jukwaa vilivyo.
Omy Dimpoz alifuata jukwaani kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile
iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nain a kusindikizwa na
wacheza show wake wanne.
Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba alifuata jukwaani na
kuimba nyimbo kadhaa na kumpisha Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa
Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT ambaye aliimba nyimbo kadhaa
ikiwepo iliyompa Tuzo ya Vifuu Utundi amabyo aliicheza vilivyo na
wanenguaji wake waili wa kike.
Baada ya Kushika AT alipanda tena Barnaba kasha kumpisha Mkali wa Tuzo za
Kili Music Award 2012 Diamond ambaye alijizolea Tuzo tatu alipanda jukwaani
kwa kishondo huku akiwatanguliza wacheza show wake.
Diamond akishangiliwa vilivyo aliimba sambamba na kucheza nyimbo zake
takriban zote huku zilizo mpa tuzo za Wimbo Bora wa Mwaka na ule wa Mawazo
uliompa Tuzo bora ya Video bora zikishangiliwa vilivyo.
Diamond ambaye ndiye anazungumzwa kwa sasa kuwa msanii ghali na bora nchini
alimudu vyema kushambulia jukwaa na kuwafanya mashabiki muda wote mikono
kuwa hewani.
Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofabnya
ziara na waliobahatika kufika jijini Mwanza lilifungwa na Roma Mkatoliki
a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa za
mistaari ya maandiko.
Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo
wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa
huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.
Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo Mkoani
Kilimajaro katika mji wa Moshi na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru
mashabiki wao wa Mkoani Dodoma kwa kuwapa kura za ushindi.
Tupo pamoja mama wa michezo
ReplyDelete