KOCHA Mkuu wa timu ya taifa, Kilimanjaro Taifa Stars, KimPoulsen amesema kikosi chake kina kazi kubwa katika mechi ya kesho
dhidi yawenyeji Msumbuji, lakini ushindi ni lazima.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Msumbiji ‘Mambas’.
Mechi ya kesho itachezwa kwenye Uwanja wa taifa wa Zimpeto jijini
hapa.
Akizungumza jana
mjini hapa, Poulesen raia wa Denmark alisema wachezaji wake katika morali ya hali ya juu na wanachotaka
ni kushinda mchezo wa kesho.
“Msumbiji ni timu nzuri, wanacheza kwa kasi na kila kitu
nimekifanyia kazi.
Ninaamini tutafanyaa vizuri kikubwa ni kufuata
maelekezo ya kila tunachotakiwa kufanya,” alisema Poulsen.
Stars ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia
bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilitua hapa Ijumaa na kufanya
mazoezi juzi na jana ilitarajia kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi
hiyo ya
kuwania kucheza KOmbe la Maataiafa Afrika lililopangwa
kufanyika nchini Afrika Kusini, Januari mwakani.
Kwa upande wa nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema ana
imani kuba na kikosi chake ambacho kitacheza kwa kujituma.
Morali yetu iko juu na kitu muhimu
ni ushindi.
Hakika ushindi ndiyo kitu muhimu,” alisema.
hiyo kesho ni ushindi.
“Tunawaheshimu haina maana tunawahofia, tunataka ushindi.
Tunajua bila ushindi hatutakuwa katika nafasi nzuri, tutajitahidi kadiri
ya uwezo wetu kufanya vizuri,” alisema.