WAKATI zoezi la uchukuaji
fomu za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
limewataka wanachama wake kufuata kanuni za uchaguzi zilizowekwa na shirikisho
hilo.
Hatua hiyo inafuatia baadhi
ya wanachama wa klabu ya Yanga kukiuka kanuni hizo kwa kutoa taarifa potofu
kuhusiana na uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za zilizowazi utakaofanyika Julai
15mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ya TFF Deogratius Lyatto alisema jana kwamba uchaguzi huo ni kwa ajili
ya kuziba nafasi za viongozi ili kutimiza akidi na si kwa ajili ya kuchagua
upya viongozi kama inavyoenezwa.
“Kuna upotoshwaji unafanywa
na baadhi ya wanachama kuhusiana na uchaguzi huu, napenda ieleweke kuwa,
uchaguzi huo utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja
aliyefariki dunia, hivyo wanachama wa Yanga wafahamu hilo na
kuzingatia,”alisema.
Mbali na hilo, Mwenyekiti
huyoa lisema kwamba viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda
uliosalia kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo hiyo viongozi hao
watamaliza muda wao wa miaka minne mwaka 2014.
“TFF inaamini kuwa wajumbe wa
kamati ya uchaguzi wa Yanaga wqatatekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba
na kikanuni kuhakikisha kwamba klabu hiyo inajaza nafasi zilizowazi katika mkutanio mu wa uchaguzi kwa kipindi
kilichobaki cha mamlaka ya kamati ya utendaji (ibara ya 29 ya Katiba ya
Yanga),”alisema.
Kwa mujibu wa Katibu wa
kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili, zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu
litamalizika Juni 6, huku Juni 7 hadi 13 kamati itapitia majina ya walioomba kugombea na kutangaza
majina yao, wakati juni 14 hadi 18 itakuwa ni kipindi cha kupokea pingamizi.
Aidha, Juni 19 hadi 23
utafanyika usaili na kutangaza matokeo, wakati juni 24 hadi 26 itakuwa ni
kipindi cha kukata rufaa, juni 27 hadi julao mosi kamati ya uchaguzi TFF
itasikiliza rufaa kama zipo, huku Julai 2 yatatabgazwa majina na kampeni kuanza
hadi julai 14.
Uchaguzi huo unafuatia
kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga baada ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama
wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kutokana na kushindwa kuiletea
mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi wake.
Pia nafasi ya Makamu
mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi michache
baada ya kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe Theonest
Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.
Uchaguzi huo pia utajaza
nafasi za Wajumbe walioachia ngazi ambao
ni pamoja na Mzee Yusuf, Charles Mgondo na Ally Mayay.
Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe
wanne, Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada
ya uchaguzi wataungana na viongozi wapya na kuteua wajumbe wengine watatu kwa mujibu wa
katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed, Mbaraka Igangula
na Pascal Kihanga kujiuzulu.
.