TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mcheza sinema toka Marekani
Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya
Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon
zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.
Ujio wa Lorenz ambaye
amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big
Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake
umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.
Akizungumza na waandishi wa
habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia
kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya
kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya
kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania.
“Nimekuwa nautangaza sana
ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi
wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz
ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz
alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi
nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
“Sasa nimeona mwenyewe kwa
macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya”
alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New
York City linalofahamika kama jiji
la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika
hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered
mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru
Park.
Mji wa Moshi na viunga vyake
vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja kushiriki
kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza Tanzania nchini
Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances mwaka
1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania nchini Misri.
Mbio hizi zimejijengea
umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na
Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa
nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa
duniani wakati jarida la Forbes la Marekani
lenye wasomaji wengi duniani limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana
Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.
Mbio hizi hukimbiwa na
watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania
kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro
Marathon zinajulikana kama 7 continental races
zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia.
Ratiba ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho
ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha Upendo kinachoendeshwa na
watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na watoto hao na kuwasomea hadithi
mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne
ya ishirini wa Marekani.
Siku ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC
ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya
jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na
wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili
tarehe 24 juni.
Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
--
Mt. Kilimanjaro Marathon
Technology House
35-38 Ghalla Road
Moshi – Tanzania