MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba wamefuta
mpango wa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wao Dan Mrwanda (Pichani) anayecheza soka la
kulipwa katika klabu ya DT Long An ya Vietnam , imfahamika.
“Tumeamua kuachana na Mrwanda kwani pamoja na kutaka dau la
mil.12, pia ametaka mkataba atakaousaini umruhusu kwenda nje iwapo atapata timu
ya kuichezea, kitu hicho hatukubaliani nacho kwani ni sawa na kutupa
fedha,”alisema kiongozi huyo.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo
wakiwemo nyota wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi
na michuano ya kimataifa wameanza mazoezi.
mwisho