WADHAMINI
wakuu wa timu ya soka ya Tanzania ,
Kili Taifa Stars, kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha
Kilimanjaro Premium Lager, inaamini timu hiyo chini ya Kocha Kim Poulsen,
itafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Hayo
yamedokezwa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (pichani), wakati
nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja akimtambulisha rasmi kwa wachezaji na
viongozi wa timu hiyo katika chakula cha mchana.
Kavishe
alisema, kwa mujibu wa maelezo yaliyomfikia, wachezaji wa Stars walicheza kwa
juhudi kubwa katika mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Ivory Coast , mjini Abidjan , licha ya kufunbgwa mabao 2-0.
“Nimeelezwa kuwa mlicheza vizuri kwa kujituma
na tulikosa nafasi nyingi za kufunga magoli,” alisema Kavishe huku akishangiliwa
na wachezaji.
Alisema kampuni yake inaamini huu ni mwanzo tu
na timu ina nafasi ya kupata matokeo mazuri zaidi katika mechi zijazo hasa ya
Jumapili dhidi ya Gambia
katika vita ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka
2014.
“Lazima tuwafanye watanzania wajione kama sehemu ya timu ya taifa ili watushangilie wakati
tunacheza ili ifike wakati walie na sisi tunapolia na wacheke na sisi
tunapocheka,” alisema
Aliwaasa
wachezaji kuwa karibu na wananchi ili waweze kujisikia kama sehemu yao kwani
watanzania
wana matumainai makubwa na timu yao ,
hivyo ni jukumu la wao wachezaji kuendelea
kuwapa matumaini kwa kujituma uwanjani.
Kavishe alisema amefurahishwa na jinsi kocha wa sasa ameweka nidhamu katika
timu ya taifa kwani ni jambo muhimu kwa mchezaji wowote.
Naye
kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen aliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa udhamini wake mnono
kupitia kinywaji chake cha Kilimanajro Premium Lager na kuongeza uwa timu
haiwezi kuwa imara bila udhamini wa uhakika.
“Kwa
sasa tunaweza kufanya mipango ya muda mrefu bila wasiwasi wowote kwa sababu
udhamini ni wa uhakika,” alisema.
Poulsen
alisema amefurahishwa sana
na udhamini wa Timu ya Taifa na kwamba viwango vya wachezaji vinazidi kuimarika
siku hadi siku.
Mpaka
sasa Timu ya Taifa imecheza mechi mbili tangu itangazwe rasmi ya kwanza ilikuwa
ya kirafiki dhidi ya Malawi
ambapo timu zote mbili zilitoka sare ya bila kufungana na mechi ya pili ilikuwa
dhidi ya Ivory Coast
ambayo ilikuwa mchujo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia ambapo Stars ilifungwa
2-0.
Jumapili
hii Stars inatarajiwa kucheza na Gambia katika mchujo wa kufuzu
kucheza Kombe la Dunia.