Nyanda ambaye anagombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji alipata kuwa mchezaji wa
Yanga katika miaka ya 2000, pia aliwahi kuzichezea timu za Abajalo, Barcelona na
Toto African zote za Mwanza.Pia alikuwa waziri wa Michezo katika Chuo cha Elimu
ya Biashara (CBE) kwa vipindi viwili wakati anasoma.
Nyanda ambaye kwa sasa ni
mfanyakazi wa benki ya NMB kama Ofisa Biashara anasema ameamua kugombea Yanga
ili kuifanya iwe imara, kuwafanya wanachama wajitambue, kuhakikisha timu
inakuwa bora na uchumi madhubuti.
Anasema iwapo atachaguliwa
kushika nafasi hiyo kwa kushirikiana na wenzake atakahikisha Yanga inapata
mapinduzi makubwa katika mambo hayo na hasa ikizingatiwa kuwa ni klabu konge
katika ukanda wa Afrika MAshariki na Kati.
“Nawaomba wanachama wa Yanga
wanichague kwa maendeleo ya klabu na soka la Tanzania kwa ujumla kwani
ninafahamu udhaifu wote hivyo nitaushughulikia ipasavyo,”anasema.