Sara Ramadhan na ofisa wa idara ya habari Maelezo
MGOMBEA
wa uenyekiti katika uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika
Jumapili
jijiji Dar es Salaam ,
Sara Ramadhani amepinga kuenguliwa kwenye uchaguzi mdogo
wa
Klabu ya Yanga kulikofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania
(TFF).
Sara,
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga katika uongozi ulioingia madarakani Julai
18,
2010,
amechujwa na kamati hiyo kwa hoja ya kutokidhi masharti ya kuomba uongozi kwa
mujibu
wa Ibara ya 10(4) na (5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Kwamba,
Sara hakukidhi matakwa ya kanuni hiyo iliyoainishwa kwenye fomu namba
1,
kwa kutojaza fomu na kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za kugombea, uamuzi
ambao
umesisitizwa pia na TFF.
Akizungumza
kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO,
jana, Sara alisema bado ni mgombea
halali katika klabu hiyo kwani kitendo cha Shirikisho hilo kumzuia, ni kuingia mamlaka ya Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa.
“Nimekuja
kuwaeleza kuwa mimi bado ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika klabu ya
Yanga,
sitambui hatua ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuniengua, inajipa mamlaka yasiyo
yake, inaingilia mambo ya klabu, ikitambua kuwa Yanga si ya soka pekee,”
alisema Sarah.
Alisema
inachofanya kamati ya uchaguzi ya TFF, ni kujipa mamlaka yasiyo yake kwa
kuingilia mambo ya Yanga huku ikijua kuwa klabu hiyo ni ya michezo na sio ya
soka pekee.
Aliionya
kamati hiyo ya uchaguzi ya TFF kwamba iiache kamati ya uchaguzi ya Yanga
iendeshe
zoezi
hilo la
uchaguzi kwa uhuru sio kuingilia na kupinga kile ambacho kimeridhiwa na kamati
ya uchaguzi ya Yanga.
“Kamati
ya uchaguzi ya TFF iache kuingilia mambo yasiyo yake, mimi sikutaka kupeleka
vyeti kama walivyotaka kwa sababu wao
hawahusiki na uchaguzi wa Yanga, uamuzi wa kamati ya uchaguzi ya Yanga ndio wa
mwisho,” alisema.
Aidha,
aliishutumu TFF kwa kuminya haki za kisheria kwa kupiga marufuku wadau wake
kutokwenda mahakamani, nahodha wa Chelsea ya England , John Terry ameshitakiwa
kwa tuhuma za kumfanyia vitendo vya kibaguzi Anthony Ferdinand wa Queens Park
Rangers.
“Unajua
TFF inatumia udhaifu wa Watanzania kutofuatilia mambo, masuala ya soka
hayajazuiwa kwenda Mahakamani, Terry amefikishwa mahakamani tena kwa kosa
lililofanyika ndani ya uwanja, mbona Fifa-(Shirikisho la soka la Kimataifa),
limebaki kimya,” alihoji Sara.
Hata
hivyo, alipoulizwa kuwa haoni kama jambo hilo
lilipaswa kupingwa mapema kwa katiba za Klabu kutofuata mwongozo wa TFF, Caf na
Fifa, alisema kila jambo lina wakati wake na ndio sasa.
“Hivi
sisi tukisema tufuate matakwa ya kila mchezo itakuwaje, riadha watuambie hivi,
TFF watake tufanye vile, ngumi nao watake hivi, tujiulize itakuwaje? sisi ni
klabu ya michezo sio klabu ya soka,” alisema.
Wengine
waliochujwa na kamati ya Uchaguzi ya TFF, ni Shaaban Katwila, Ahmed Waziri Gao
na Ramadhani Kampira wakiungana na Ally Mayay, Abdallah Sharia, Jamal Kisongona
Mohamed Mbaraka waliochujwa na Kamati ya uchaguzi ya Yanga.