Manyama anasema ameamua
kujitosa kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kuifanya Yanga ijitegemee na
kuondokana na hali ya kusubiri ufadhili.
Anasema iwapo atafanikiwa
kutwaa nafasi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha wanaifanya
Yanga inakuwa tishio ndani na nje ya nchi kwa kushinda mataji mbalimbali.
Manyama ambaye ni
mfanyabiasha, anasema aanauzoefu wa kuongoza kwani kwa miaka 15 amekuwa
akiisaidia Yanga kwa namna moja ama nyingine.
“Mimi kama mfadhili wa tawi la Yanga Kigogo nadhani ni
wakati wangu wa kuleta utaalamu wangu wa kuongoza katika Yanga yetu...naombeni
kura zenu.