WANACHAMA wa Yanga ni
nani asiyemfahamu Binkleb kutokana na michango ya kuinusururu klabu hiyo pindi
ilipotetereka, ikiwemo kugharamia kambi ya wachezaji baada ya viongozi kujivua
gamba.
Kama hiyo haitoshi
Binkleb ndiye aliyemsajili kiungo wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima, pia
kwa kushirikiana na swahiba wake Seif Ahmed ‘Magari’ wamemleta kocha wa sasa,
Mbelgiji Tom Saintfiet na mengineyo.
Bin Kleb anasema ameamua
kujitosa kuwania Yanga ili kuendeleza mpango wake wa kuisaidia Yanga ili iweze
kupata mafanikio ikiwemo kushiriki hatua ya nane bora ya michuano ya Afrika.
“Ninataka ndani ya miaka
miwili Yanga iwe katika matawi ya juu katika bara la Afrika na hilo
litaambatana na usajili mzuri na uwekezaji katika timu za vijana na makocha
waliobobea,” anaongeza.
Mbali na hilo, mgombea
huyo anasema iwapo atafanikiwa kutwaa nafasi hiyo, kwa kushirikiana na viongozi
wenzake atahakikisha kunakuwepo na uwazi wa mapato na matumizi kwa wanachama
kila baada ya miezi mitatu.
“Pia nitasaidiana na
wenzangu kuleta mfumo wa kuendesha miradi endelevu kwa manufaa ya klabu ili
iondokane na mfumo wa sasa wa utegemezi,” anaongeza.
Aidha Bin Kleb anasema
iwapo atapata fursa ya kuongoza Yanga pia atashirikina na viongozi wenzake
kutengeneza miundombinu ikiwemo kuweka nyasi bandia katika Uwanja wa Kaunda
hali ambayo itaziwezesha timu zao kufanya mazoezi kikamilifu.
“Nachukua fursa hii
kuwaomba wanachama wa Yanga kunichagua ili niendeleze mambo mazuri,” anaongeza.