Kozi ya makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji
mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza
leo (Julai 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Msimbazi
Center , Dar es Salaam .
Wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) ndiyo wanaoendesha kozi hiyo iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Angetile Osiah.
Kozi hiyo itakayomalizika Julai 15 mwaka huu inashirikisha
washiriki 35, na mwendelezo wa ile ya awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka
jana jijini Dar es Salaam .
Gouinden Thandoo kutoka Mauritius ni mmoja wa wakufunzi wa
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wanaoendesha kozi hiyo.