Michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu, screen kubwa iliyoko
uwanjani itatumika kwa matangazo ya biashara na ujumbe mbalimbali kwa washabiki
watakaoshuhudia mechi hizo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha
kampuni na wadau mbalimbali wanaotaka kuweka matangazo yao wakati wa michuano hiyo itakayoshirikisha
klabu kumi na moja kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Muda wa kurushwa matangazo hayo yanayotakiwa kuwa kwenye
mfumo wa DVD ni kabla ya mechi kuanza, wakati wa mapumziko na baada ya mechi.
Matangazo hayo yanatakiwa kuwa ya sekunde 60 (dakika moja) au sekunde 30 (nusu
dakika).