Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:
Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%
Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)
kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama