Yusuf Manji -Mwenyekiti mpya wa Yanga
Clement Sanga- Makamu Mwenyekiti
Abdallah Bin Kleb- Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
George Manya-Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Aaron Mwinula Nyanda-Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Clement Sanga- Makamu Mwenyekiti
Abdallah Bin Kleb- Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
George Manya-Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Aaron Mwinula Nyanda-Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza
uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15
mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar
es Salaam .
Ushindi waliopata wajumbe wapya sita waliochaguliwa kuingia
kwenye Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wanachama wa Yanga
waliohudhuria uchaguzi huo walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya
Utendaji ya Yanga ambayo hivi sasa ina vinara wapya, na kwamba wana changamoto
kubwa ya kuhakikisha wanaendesha shughuli za klabu hiyo kwa kuzingatia katiba
na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga chini ya
Jaji Mkwawa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na
kanuni.