Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa timu ya soka ya Yanga,Tom Saintfiet ameeleza kwambaamejiandaa kutoa onyo kali kwa timu za ligi kuu kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya Africa Lyon.
Kocha huyo ameeleza hayo juzi wakati akizungumza na gazeti hili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola,Dar es Salaam kwamba amejipanga vyema kuutoa onyo hilo kupitia kwa washambuliaji wake.
Alisema baada yak ufanya mazoezi ya nguvu ana imani wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya ligi kuu ambapo kwanza waanza kwa kutoa kupambana na African Lyon keshokutwa.
Mchezo huo wa kirafiki umeandaliwa na Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA)kwa kushirikiana na Kampuni ya Vannedrick(T)Ltd utafanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo wa kesho,kocha huyo ameeleza kwamba anatarajia kuwapanga Said Bahanuzi ambaye atashrikiana vyema na wakali wengine wakiwemo Hamis Kiiza,Haruna Niyonzima,Didier Kavumbagu.
Hata hivyo,kocha huyo amekiri kwamba hivi sasa mshambuliaji wake Jerryson Tegete naye ni moto wa kuotea mbali kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao.
Alisema baada ya mchezo huo,kikosi chake kitaondoka nchini siku ya Jumanne kwenda Rwanda ambapo watacheza michezo kadhaa ya kirafiki kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya kuanza ligi kuu msimu ujao.
Viingilio katika mchezo huo ni,VIP A wakati VIP B ni shilingi 10,000 huku upande wa viti vya rangi ya machungwa ni shilingi 5,000 na mzunguko shilingi 3,000 na kuwataka mashabiki wa soka kufika kwa wingi ili kuona jinsi kikosi chao kitakachotoa dozi kwa Yanga.