TIMU ya Vijana ya Simba
‘Simba B’ leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya
kwanza ya Banc ABC Sup8r baada ya
kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 4-3.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ,
Simba ilionekana kutawala kila idara katika mchezo huo ambapo vijana hao
waliwahenyesha wapinzani waoMtibwa.
Edward Christopher ndiye alianza kuiandikia Simba bao
la kwanza katika dakika ya 12 alipoitendea haki pasi ya Haruna Athuman na kumuuza kipa wa Mtwiba, Shaban Kado langoni
mwake.
Dakika ya 32 Shaban Kisiga aliisawazishia
Mtibwa kwa bao la mkwaju wa penalty ambapo mwamuzi Hashim Abdallah kuamuru hivyo
kutokana na mchezaji wa Simba Omary
Salum kumchezea vibaya Jamal Mnyate wa Mtibwa.Bao hilo lilidumu hadi timu hizo
zibnakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa
timu kucheza kwa umakini huku Simba wakicheza mpira wa akili na kuwachosha
wakata miwa hao wa Mtibwa na kuwafanya
kucheza mpira wa kutumia nguvu.
Christopher aliiandikia tena
Simba bao la pili katika dakika ya 52, akimalizia krosi ya Rashid Ismail, kabla
ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya 56 kupitia Kisiga aliyepiga shuti kali
nje ya 18 na kumshinda kipa wa Simba.
Simba ilipachika bao la tatu
katika dakika ya 66 likipachikwa na Haruna Athuman mara baada ya kuwatoka
mabeki wa Mtibwa, kabla Hassan Seif kuitumia safu faulo na
kusawasazisha katika dakika ya 73.
Dakika 90 za mchezo huo ambao
ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dh.Fenella
Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi,zilimazika kwa timu hiyo kwenda sare ya
mabao 3-3 hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30.
Alikuwa ni Christopher tena
ambaye aliifungia Simba bao la ushindi katika dakina ya 102 alipomalizia kazi
safi ya ia kazi safi ya Frank Sekule na
kufanya bao hilo lidumu hadi dakika ya 120 na kuifanya Simba kushinda kwa mabao
4-3.
Kwa ushindi huo, Simba
imepata milioni 40 pamoja na medali , huku Mtibwa ikiondoka na shilingi mil 20
pamoja na medali.
Aidha, shujaa wa Simba
Christopher alizawadiwa sh milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora baada ya
kufunga mabao 7, huku kipa wa Simba Abuu Hashim alizawadiwa sh milioni 2.5 kwa
kuwa mchezaji bora.
Michuano hiyo ilianza kutimua
vumbi Agosti 8 na kuzishirikisha pia timu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam
Fc,Polisi Morogoro kwa upande wa Bara, huku Visiwani iliwakilishwa na Mafunzo ,Zimamoto, Mtende na Super Falcon.
Simba:Abuu Hashim, William
Lucian, Omary Salum, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Haruna Athuman,
Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Edward Christopher na Ramadhan Singano/Fank
Sekule.
Mtibwa Sugar:Shaban Kado,
Malika Ndeule, Yusuf Mguya, Salum Swedy, Salvatory Ntebe, Babu Ally, Jamal
Mnyate, Awadh Juma, Juma Javu, Shaban Kisiga/Hassan Seif na Vicent Barnabas.
Hongera kwenu !
ReplyDelete